Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amesema kwamba kwa ndani ya Miaka mitatu ana Album 3 kitu ambacho hakuna Msanii wa Generation yake ambae ameshawahi kufanya.

Mbali na hivyo Harmonize amesema huwenda Album yake ya Made for Us inayotarajiwa kutoka Oktoba 28,2022 siku ya Ijumaa ndio ikawa Album ya Mwisho ya Kiswahili.

Albam hiyo itakuwa ni albam ya tatu kwa msanii huyo toka alipoanza kufanya muziki chini ya WCB mpaka sasa kumiliki lebo yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la Konde Gang.

Harmonize amewataka mashabiki wake kuisapoti albam hiyo ambayo inatarajia kutoka mwezi huu tarehe 28 siku ya Ijumaa baada ya kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *