Promota wa show kutoka Nchini Nigeria, Dee Jay Chii ambaye sauti yake hiyo analalamika kuwa msanii Harmonize ameshindwa kufanya show nchini Canada baada kulipwa kiasi cha $10,000 (zaidi ya Milioni 23)
Dee Jay Chii anasema kuwa tayari walishafanya makubaliano Harmonize na akalipwa lakini aliingia mitini na akawa hapokei simu mpaka muda huu.
Harmonize alitakiwa kutumbuiza kwenye miji mitatu nchini Canada kuanzia 07 – 10 Oktoba mwaka huu kutokana na maelezo hayo.
Kwa mujibu wa promota huyu anasema kwamba tayari jambo hili amelifikisha mikononi mwa polisi hapa Tanzania na linafanyiwa kazi.