Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amewashangaa wasanii wanaojitoa kwenye Lebo ambazo zimewafanya kuwa wasanii wakubwa na kuwaambia kuwa wasanii ambao wapo njee ya Lebo wanamaisha magumu.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Nuh amesema kuwa alikuwa na mpango wa kuachia EP yake lakini imeshindikana kwani kila mtu ana mtu wake.
“Mimi Nilitangaza Kuachia EP ila Mpaka sasa ishakua BP kwangu mana Kila mtu Ana Mtu wake ‘Nawaonea huruma sana Mnaotoka kwenye Usimamizi.
Mwanamuziki huyo kwasasa anatarajia kuachia EP yake baada ya kukamilika kwa nyimbo kwenye EP yake hiyo mpya kabisa.