Uongozi wa Konde Music Wordwide leo umetangaza kuagana na kusitisha mikataba ya Wasanii Ally Kili Omary (Killy) na Rashid Daudi Manga (Cheed) kwasababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo Konde Music.
Taarifa rasmi ya Konde Gang imeeleza yafuatayo “Wasanii hawa watakuwa Wasanii huru na kufanya kazi na kuingia mkataba na Kundi au Mtu yeyote na kuendeleza kazi zao.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa kwakuwa tunaamini ni Vijana Wasanii wenye uwezo mkubwa wa kufanikiwa katika safari ya muziki”
Pia taarifa hiyo imeendelea kwa kusema “Aidha, Konde Music Worldwide haitahusika na jambo lolote litakalohusisha Wasanii hawa kuanzia leo.
Mwisho taarifa hiyo imemaliza kwa kusema kuwa tunapenda kuwashukuru Killy na Cheed Kwa ushirikiano wao katika kipindi chote cha kuwa pamoja na tunawatakia mafaniko mema katika kazi zao hapo baadaye.