Wakili wa wasanii Pharrell Williams na Robin Thicke amekata rufaa mpya dhidi ya adhabu ya kulipa mamilioni ya dola kwa familia ya marehemu Marvin Gaye.
Kesi hiyo ya kuigwa kwa wimbo Blurred Lines wa Gaye ilitolewa hukumu mwaka 2015.
Wazee wa baraza wa mahakama ya Los Angeles waliamua kuwa ngoma ya Pharrell Williams na Robin Thicke ambayo ilikuwa miongoni mwa ngoma bora sana za mwaka 2013 ilivunja sheria za haki miliki ya ngoma ya Marvin ya 1977.
Familia ya mkongwe huyo ililipwa mamilioni ya pesa pamoja nakupewa haki ya kupokea 50% ya faida ya mirabaha kwa kadri kazi hiyo inavyoendelea kutumika.
Sasa mawakili waThicke na Williams amekuja na hoja mpya za kuitaka mahakama hiyo kupangua hukumu ya awali.
Mawakili hao wanadai kuwa kesi hiyo haikupaswa kwenda mahakamani na hivyo hukumu yake inapaswa kutenguliwa kwa mujibu wa kile walichokiita kama ‘a cascade of legal errors’ ambayo ni mkusanyiko wa makosa mengi ya kisheria.
Lakini hata hivyo mwanasheria wa familia ya Marvin Gaye, Richard Bush amepinga hoja hiyo na kusema: ‘Hoja nyingi katika hizi wanazozitoa sasa tayari zilishakataliwa na hakimu wa wilaya na muhtasari wa utangulizi wetu wa kujibu hoja hizi utakuwa na kile tunachoamini kuwa ni majibu kwa kila hoja watakayoitoa’.
Nini kitatokea?