Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amedai kujuta kuiingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na Paula ambaye ni mtoto wa Kajala na P Funk Majani.
Suala la kumpenda Paula lilikuwa linamyima amani ya nafsi na akili na aliamua kuchukua uamuzi mgumu kisha kuanza safari ya matumaini ya kuvunja penzi lake na binti huyo wa kambo wa msanii Harmonize.
Pia Rayvanny anawashauri watu kutofanya mfananisho wa mapenzi na chakula kwani ni vitu viwili tofuati.
Rayvanny ambye ni baba wa mtoto mmoja, miaka michache nyuma alimbwaga aliyekuwa baby mama wake, Faima lakini sasa amerejesha majeshi wanamlea mtoto wao pamoja.
Kabla ya kuthibitisha kuachana na Paula, Rayvanny alisema hakuna mtu anayepaswa kuwachanganya kutokana na kuona ukweli wa mambo.