Aliyekuwa mpiga picha wa Diamond Platnumz ambaye kwasasa ni mwanamuziki, Lukamba amefunguka na kumtaka H Baba aache tabia ya kumchonganisha na bosi wake huyo wa zamani.
Lukamba amemwambia H Baba kuwa yeye anamjua na Kumkubali Diamond kuliko yeye hivyo Asitake kuleta Uchonganishi kati yao.
Kupitia Instagram ya Lukamba Ameandika.
“BRO ME NAMJUA SIMBA KULIKO WEWE NAMKUBALI SIMBA KULIKO WEWE NA HATA YEYE PIA ANAJUA HILO …HAKUNA SEHEM NILIWAHI SEMA SIMBA AJANISAIDIA ALAFU HII KAULI KWAMBA ALITOKA VIBAYA WE UNAJUA MIKATABA YETU MMEKAZANIA KATOKA VIBAYA VIBAYA KUNASEM NISHAWAHI MVUNJIA KHESHMAAA ACHENI HIZO MWACHENI MTU AFANYE MAISHA YAKE ACHENI UCHONGANISHI”
Kauli hiyo ya Lukamba imekuja baada ya H Baba kusema kuwa Lukamba ameondoka Kwa Staa huyo kwa Ubaya na Anapadharau Palipomfikisha alipo sasa na Kumwambia kuwa Asitake Kushindana.