Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amefunguka na kusema kuwa yeye ndio alimwambia Alikiba audhurie kwenye harusi yake huku amevaa t-shirt na jeans kwa kuwa alikuwa anatoka safari.

Alikiba alihudhuria harusi hiyo huku akiwa amevalia Mavazi yasiyo Rasmi lakini Billnass amesema kuwa yeye ndio aliyemwambia Alikiba kuja vile kwenye harusi yake na Nandy.

Billnass ameendelea kusema kuwa Alikiba alimpigia simu kwasababu waliongeza mara kwa mara kuhusu harusi hiyo na alimwambia kuwa atasafiri lakini aliwahi kurudi kwa hiyo akamwambia nipo njiani narudi kwa hiyo naenda home kubadilisha nguo ndio nakuja.

Kutokana na hivyo nimeona anaweza kuchelewa aende mpaka nyumbani kwake ndio nikaamua kumwambia kuwa aje vile vile kama alivyo ndio akaja kwenye harusi kama alivyoonekana.

Amesema ‘Mimi Kwasababu Tuliongea Kuhusu Harusi Mara Ya Kwanza Akaniambia Atakuwa Amesafiri Hivyo Akawa Amewahi Kurudi Amerudi Ile Jioni Akanambia Ningefikiria Kuja Lakini Mpaka Niende Nyumbani Nibadilishe Nguo Nikamwambia Wewe Ibuka Tu Akawa Na Wasiwasi Kuhusu Mavazi Aliyokuwa Amevaa’

Pia akasema  Ndio Maana Ata Unaona Watu Wengi Walimlaumu Kuhusu Mavazi Lakini Mimi Ndio Nilimwambia Bro Wewe Njoo Tu Vyovyote Ulivyo Kwasababu Harusi Ni Siku Moja Kwahiyo Alikuja Kwa Upendo Wangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *