Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kusema kuwa kwasasa anaendelea vizuri baada ya kuugua ugonjwa wa Corona.

Alikiba Kwa Mara Ya Kwanza Tangu Atangaze Kugua Ugonjwa Wa Corona Ameweka Wazi Kuendelea Vizuri Kwasasa Tofauti Na Vile Alivyokuwa Mwanzo.

Wiki moja iliyopita mwanamuziki huyo alitangaza kusitisha kufanya ziara yake nchini Marekani baada ya kuugua ugonjwa wa Corona na kumfanya atulie nyumbani kwa kupatia matibabu.

Mwanamuziki huyo kwasasa anaendelea vizuri na yupo tayari kwa ziara yake japokuwa hajatangaza siku ya kuanza kwa ziara yake hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *