Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka The Prince amesema kuwa hamkubali kabisa na hampendi msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Alikiba.

Sakata lilianza pale wakati ana pafomu alipomaliza mashabiki waliomba apafomu ngoma yake aliyomshirikisha, Alikiba na kusema hataki kumsikia na Alikiba ni mpumbavu tu.

Mbali na hilo Baraka amezungumzia kuhusu baadhi ya Album ambazo zimetoka na je anazizungumziaje? Baraka ameeleza kuwa album ya Weusi, High School ya Harmonize na Only one King ya Alikiba ni kali sana.

Alipoulizwa kuhusu kuadimika kwa show zake Baraka ameeleza kuwa kwa sasa anafanya show za harusi na analipwa kwa dola.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *