Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu ametoa uzoefu wake wa Show ambayo Aliwahi Kuogopa Zaidi Katika Maisha Yake Ya Muziki Ambayo Ameitaja Kuwa Ni Show Ya I am Zuchu  Launching Aliyofanya Mlimani City Alipo Tambulishwa Rasmi Na Label Yake Ya WCB.

“Siku Ya Kwanza Nilikua Naenda Kuperform I am Zuchu Launching Watu Walikuwa Wanapitia Kipindi Cha Korona Kwahiyo Yakwanza Tulifanya Indoor Hakukuwa Na Watu So Ya Pili Ile Siku Sikulala Napenda Jinsi Boss Alivyoichukulia ‘Mbona Unaenda Pale Unaua Nakuaminia”

Na Pia Sikufanya Mazoezi Sana Nilifanya Siku Moja Tu Kesho Yake Ndio Shughuli Yenyewe Na Pia Usiku Huohuo Ilikuwa Ni Lazima Tumalizie Wimbo Wa Mauzauza Niliyo Mshirikisha Mama Yangu (Khadija kopa) Ili EP Ikitoka Na Huo Wimbo Uwepo Ndani”

“So Kulikuwa Na Vitu Vingi Vinatokea Kwa Pamoja Nakumbuka Nilikua Studio Boss Ananikazania Nimalize Wimbo Na Nilikua Naogopa Kumwambia Nimechoka Kwahiyo Alivyotoka Nikaanza Kulia Kina Mbosso Wakaanza Kunibembeleza Nilikua Nimechoka Pamoja Na Uoga Na Nilikuwa Naharisha Siku Nzima Nilikua Naogopa Sana Nikawa Nawaza Vipi Kesho Nikaperform Watanzania Wasinikubali? Kwahiyo Ndio Show Ambayo Sitakuja Kuisahau Kwenye Maisha Yangu Nafkiri Ile Show Ilinipa Uoga Ambao Sijawahi Kuupata Tangu Nimeanza Muziki”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *