Video ya wimbo wa Mama Tetema kutoka kwa Staa wa Muziki kutoka Nchini Colombia Maluma akiwa na Rayvanny imere imerejeshwa katika Mtandao wa Youtube.
Siku kadhaa zilizopita Video hiyo iliondolewa katika Mtandao huo kwa Madai ya Hati miliki kutoka kwa Salmin Kasimu maarufu kama S2Kizzy Ambae inasemekana ni Mtaarishaji wa muziki.
Wimbo huo kwasasa unapatikana Youtube kama kawaida baada ya sintofahamu kwa wiki kadhaa kutokana kuondolewa Youtube kutokana na Hakimiliki.
Inasemekana kuwa wimbo huo uliondolewa kutokana na madai ya mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, S2Kizzy ambaye ndio aliyetengeneza wimbo huo.