Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ametangaza kusimamisha Tamasha lake la Nandy Festival kutokana na sababu zake za kiafya zinazotokana na ujauzito aliokuwa nao.

Tamasha hilo awali ilitakiwa kufanyika katika Mikoa Mitano Lakini Kutokana na Hali yake ya Kiafya imefanya kuishia kufanyika katika Mikoa Miwili Pekee Ruvuma (SONGEA) na Jijini Mwanza.

Kupitia ukurasa wa Instagram Amethibitisha hilo kwa kuandika… “KWANZA AHSANTEN SANA WAKAZI WA SONGEA, MWANZA NA MIKOA MINGINE KWA UJUMLA PILI WASANII WENZANGU, ONLINE MEDIA, RADIO NA WAANDISHI WOTE MLIOKUWA SEHEM YA NANDY FESTIVAL PIA MANAGEMENT NA TEAM YANGU NZIMA.

Pia ameandika KIPEKEE WADHAMINI NA WADAU WOTE AMBAO NI SEHEM YA MAFANIKIO YA TAMASHA HILI !! INSHALLAH KWA UWEZO WA MUNGU TUKUTANE NANDY 2023 TUKO VEREE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *