Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu amesema kuwa kuna wakati kwenye kazi zake, anajitolea mhanga na kubuni vitu ili kujifunza vitu tofauti na kukua zaidi kimuziki kama alivyofanya Simba Day.

Zuchu amesema kitendo cha kushuka na kambi kwenye tamasha la Simba Day iliyofanyika Agosti 8, 2022 lengo lake lilikuwa ni kuacha historia kwa mashabiki.

Zuchu amesema kuwa “kwani tayari nilikuwa nimefanya mazoezi kama mara mbili, lengo langu ilikuwa ni kuzunguka na kamba uwanja mzima ili kuwafikia mashabiki wote, maana kukimbia unaweza usiyafikie maeneo mengine na ukawakwaza baadhi,”.

Pia amewaondoa wasiwasi mashabiki wanaodhani wana bifu na msanii mwenzake Nandy kwamba wanawasiliana tofauti na picha ya mashabiki wanaowashindanisha kimuziki.

Zuchu ni msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri kwasasa kutokana na kazi zake kufika mbali kwa mashabiki wake wa muziki hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *