Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tundaman ameomba msamaha baada ya kuingia kwenye jeneza wakati akifanya show kwenye siku ya Simba uwanja wa Taifa.
Tunda Man akiongozana na wasanii wenzake, Abdukiba na Stan Bakora wameomba radhi kwa watanzania na mashabiki wao Pamoja na viongozi wa dini hususani wa dini ya kikristo kutokana na kitendo hiko.
Tundaman ametanabaisha kuwa walichokifanya kwenye kilele cha sherehe za Simba Day hakikulenga kwa namna yoyote ile kudhihaki madhehebu ya dini ya kikristo na lengo lao halikuwa kusababisha mfadhaiko kwa waumini wa dini hiyo.
Tundaman aliendelea kwa kusema kuwa lengo lilikuwa ni kuonesha ubunifu katika kazi yake ya sanaa na walilenga zaidi kwenye kuburudisha huku wakiwafanyia utani watani wa klabu hiyo ya Simba ambao ni klabu ya Yanga.
Msanii Stan Bakora alidakia na kusema kwa utani: “Nadhani pia wosia ndio uliowakera sana watu wa Yanga maana wengi waliomaindi ni mashabiki wa Yanga, Ingawa ni kweli tumegusa maswala ya kiimani”.