Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kupitia Katibu Mtendaji wa Baraza Dkt. Kedmon Mapana Limekanusha vikali Taarifa za Kumfungia Msanii wa Muziki Tunda Man.

Dkt, Mapama Amesema kuwa Taarifa za Kufungiwa kwa Msanii huyo na wao wameziona katika Mitandao ya Kijamii lakini hawajafungia Msanii yoyote.

“Taarifa na sisi tunaziona katika mitandao ya kijamii kuwa tumemfungia Msanii lakini sisi kama Baraza la Sanaa la Taifa hatujamfungia Msanii yoyote kwahiyo nataka niliweke sawa Kilichopo hapa kwetu sisi ni kuhusu matumizi ya Jeneza na Msalaba kwahiyo inaonekana kwa upande wa wakristo malalamiko hayo yanaendelea ambayo na sisi tumeyapata na tunayafanyia kazi”

“Inawezekana watu wanaona Baraza ni la Kufungia tu ndio lipo vichwani Mwao sisi kazi yetu hatutaki kufungia Tunataka wasanii wawe wabunifu lakini wafanye sanaa kwa ubunifu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *