Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka rekodi nyingine ya kulipwa pesa nyingi za shoo ndani ya muda mfupi.
Diamond alikuwa mmoja wa watumbuizaji katika hafla ya Mgombea Urais wa Kenya, Raila Odinga katika Uwanja wa Kasarani nchini humo.
Diamond alitangaza ratiba yake na kusema kwamba Jumamosi angetumbuiza nchini Kenya kabla ya kujiandaa kwenye matamasha mengine makubwa mwishoni mwa mwezi huu nchini Canada.
Diamond ambaye alikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya birthday ya binti yake, Tiffah Dangote alikodisha ndege binafsi akiambatana na binti yake huyo ambapo alikwenda kwenye shoo hiyo ambayo aliifanya kwa dakika 30 tu kisha akavuta kiasi hicho cha pesa.
Diamond alichukua tena ndege binafsi ambayo ilimrejesha yeye na Tiffah nchini Afrika Kusini kuendelea na pati ambayo ilikuwa ni kufuru tupu.
Diamond alitumbuiza Nairobi mara ya mwisho mnamo Desemba 2018 wakati wa Tamasha la Wasafi Festival kuadhimisha sherehe za Mwaka Mpya ambapo ilikuwa imepita miaka mine bila kufanya shoo Nairobi.