Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa mahaba anayopewa na mumewe Billnass katika maisha yao ya ndoa ni Zaidi ya upendo.
Nandy ambaye ni mama kijacho ame kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza ni kiasi gani kwa sasa anaenjoy kwenye ndoa kutokana na mahaba mazito anayopatiwa na mumewe huyo huku akimtaka apunguze kidogo
Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika Nyie ndoa ikiwa mpya ndo mapenzi yanazidi hivi??? Jamaaaani nimetepetaaaaaa Billnass jamaaan mume wangu punguza mapenzi jamani utaniua.”
Nandy na Billnass wana takribani mwezi mmoja tangu wafunge ndoa yao Julai 16, 2022 na sasa wanatarajia kupata mtoto wa kwanza.