DJ wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Rommy Jones almaarufu RJ the DJ kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu sakata la picha za utupu wake kuvujishwa mitandaoni na mwanaharakati mmoja wa kimitandao kupitia ‘app’ yake.

RJ amechukua fursa hiyo pia kuwaomba radhi mashabiki zake na wote waliokwazika na kitendo hicho akisema kwamba hajui zilimfikiaje mwanaharakati huyo ila anahisi ni fundi wa simu alizivujisha baada ya kumpelekea simu kuitengeneza.

“Zile picha zilizovujishwa na … (anamtaja) ni za muda mrefu, nilirekodi nilikuwa nimelewa na sijui nani aliamua kuzivujisha. Kuna mtu alipigia simu miaka mitatu minne nyuma alinipigia akaniambia: “Nina picha zako za utupu, ili nisizisambaze nitumie milioni moja nizifute”, mimi nikashtuka nikamwambia sina pesa.

“Ile simu niliyokuwa natumia mwanzo iliharibika nikaipeleka kwa fundi ili aitengeneze, ni rafiki yangu yupo Mwenge, baada ya jamaa yule kunitumia picha zile nikaripoti Polisi Oysterbay nikapewa RB, akawa anatafutwa mara yuko Buguruni mara yupo Mbezi.

“Baadaye akanitumia zile picha, ikabidi nimtumie mke wangu kumuuliza kama kwenye simu kuna hizo picha akakataa, nikamcheki fundi wangu kumuuliza kama ile simu ameiuza akasema hapana ila amei-flash, nikaenda kwake nikahakikisha kweli ame-flash hakuna picha yoyote,” RJ the DJ alisema.

Rommy amewaomba radhi wote kuanzia familia yake ambayo ni mke wake, ndugu zake na pia mashabiki wa Wasafi kwa kitendo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *