Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso amethibitisha kuzaa na aliyekuwa mke wa msanii Abdukiba huku akidai kwamba hakuwa akijua kuwa mwanamke huyo aliolewa na Abdu Kiba.

Mbosso na Abdukiba waliwahi kuwa marafiki kabla hajahamia Wasafi na hata kabla Abdukiba hajamuoa huyo mwanamke na ndoa kusambaratika.

Mbosso alisema kwamba ni kweli tukio la kupata mtoto na aliyekuwa mke halali wa Abdukiba lilitokea lakini akasisitiza kwamba ni makosa ya kina dada ambao muda mwingi huwa hawasemi kama wapo katika mahusiano pindi wanapotongozwa.

Mbosso alisisitiza kwamba hamna uhasama baina yake ya Abdukiba na kumtaja kuwa mwanake wa ubavuni kabisa.

Alisema kwamba mwanamke huyo mpaka alimfuata Kwenda tamasha alikokuwa akiburudisha Zanzibar na waliporudi Dar es Salaam wakawa wanawasiliana kwa ukaribu na mwisho wa siku matunda yakawa ni kuzaliwa kwa mtoto wa kike baina yao.

Alisema kwamba katu hakuwa anajua na kadri mahusiano yalipokuwa yanakolea ndio ndogo wake Diamond kwa jina Idd Santos alimchanua kwa kumwambia kwamba yule mwanadada alikuwa mke wa msanii na rafiki yake wa karibu, Abdukiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *