Muigizaji wa Bongo Movies, Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake hataki kujitia kero na gundu kabisa.
Uwoya amesema kuwa, kwa sasa mtu akijitia kero ni kujitakia mwenyewe kwa sababu kuna vitu vingi mno vya kumpa mtu furaha kila siku na siyo kero.
Uwoya anasema kuwa, alishasahau kero kitambo na ndiyo maana siku hizi anaachia nafsi yake kuwa na furaha tu na si kitu kingine.
Pia amesema hii ndiyo maana hivi karibuni aliamua kutafuta mtu wa kumchekesha ili roho yake ifurahi.
Mimi sitaki kero wala kujitia gundu kwa kuwaza chochote kwenye maisha yangu haya hata siku moja.
“Hii ni kwa sababu sitaki kuyatia gundu maisha yangu hata kidogo, mimi nahitaji raha siyo karaha,” anasema Uwoya ambaye kwa sasa ndiye staa wa kike mwenye mkwanja mrefu Bongo nzima.