Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars amefunguka kuhusu mahusiano yake na mwanamuziki mwenzake Marioo baada ya wawili hao kuhusishwa kutoka kimapenzi kwa muda mrefu.

Mimi Mars amefunguka na kusema kuwa Marioo ni rafiki yake wa karibu lakini hawana uhusiano wa kimapenzi kama baadhi ya watu na mashabiki wanavyosema kuhusu wawili hao.

Wawili hao walionekana wanabambiana huku wakiimba pamoja stejini kwenye show ya Muziki Mnene iliyofanyika mkoani Mtwara na kuhudhuriwa na mashabiki wengi mkoani humo wikiend iliyopita.

Wawili hao walifanya ngoma ya pamoja miezi michache iliyopita na kufanya vizuri kutokana na muunganiko wa wasanii hao kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *