Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amesema kuwa mwaka huu walitarajia wangekwenda kufanya tamasha la Nandy Festival hadi nchini Burundi, lakini atashindwa kufanya hivyo kutokana na hali yake ya ujauzito.

Nandy ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia tamasha lake hilo litakaloanza kurindima Julai 23 mwaka huu.

Pia Nandy amesema kila mwaka tamasha hilo linaendelea kukua na kwa mwaka huu walipanga liende hadi nje ya nchi kwa kulifanya nchini Burundi lakini kutokana na hali yake, hatoweza kusafiri.

Badala yake atalifanya hapa nchini na pia atafanya kwa mikoa michache tofauti na matamasha yaliyopita ambayo alikuwa akifika hadi mikoa sita.

Wakati kuhusu tamasha lake hilo la Nandy Festival alisema litaanza Julai 23 mwaka huu, na litaanzia mkoani Ruvuma huku akieleza mkoa huo utakuwa wa kwanza kushuhudia show yake akiwa tayari mke wa mtu.

Nandy anatarajiwa kuolewa na msanii mwenzake, William Lyimo ’Billnass’, ndoa inayotarajiwa kufungwa  Julai 16, mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *