Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baba Levo amemuonya Rayvanny dhidi ya kuondoka kisha kuanza kumsema vibaya Diamond kama ambavyo walifanya watangulizi wake, Harmonize na Rich Mavoko.

Baba Levo amesema endapo Rayvanny atakiuka maneno hayo basi awe tayari kwa vita vya moto maana yeye siku zote ni mpambanaji aliyejiandaa kivita, iwe ya maneno au ya kurushiana mikwara na masumbwi.

Amesema kwamba, Rayvanny ndiye aliyemleta katika familia ya WCB Wasafi na sasa ameondoka na kumuacha na kumtakia kila la kheri katika safari yake mpya kimuziki.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Kwa heri ndugu yangu Rayvanny, ulinileta Wasafi umeniacha. Mungu akusimamie kwenye kila jambo. Hakikisha husahau heshima uliyojengewa na Diamond.

Pia ameandika Yeye ndiye chanzo cha mabadiliko yetu kwenye maisha yetu ya muziki,” kwa mara ya kwanza Baba Levo anaonekana kutoa ushauri uliotukuka.

Rayvanny alitangaza kuondoka rasmi kwenye Lebo ya Wasafi na kumsifia pakubwa msanii Diamond kwa kumpa nafasi ya kuonesha kipaji chake kwa dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *