Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa amefikia hatua ya kuuanika ujauzito wake kwa sababu alichoka kumkana mwanawe kila alipokuwa akihojiwa.

Nandy amesema kuwa “Nadhani tulitaka kuweka wazi ujauzito pamoja na projekti yangu nyingine. Lakini pamoja na mambo yote hayo, bado nimebaki kuwa msanii na maisha lazima yaendelee. Siwezi kuendelea kuficha ujauzito kila wakati.

“Ujauzito ni baraka na unavyojua kuna watu wengi wanahangaika kutarajia kuwa wazazi, tunawaombea wote, kwa kazi zetu sikuweza kujificha tena kwani kazi bado zinanihitaji, nachukia kila mtu.

“Wakati nafanya mahojiano na kumkana mtoto wangu, nilikuwa nikijisikia vibaya huku nikidanganya kuwa sina mimba.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *