Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chid Benz amefunguka na kusema kuwa anataka arudishiwe pesa zake na watu ambao walilipwa kutokana na kazi zake muziki.

Chid Benz amesema kuwa kazi ziliuzwa bila ridhaa yake hivyo kwa wale wote waliohusika na kufanya hivyo anaomba arudishiwe pesa zake kwa hiyari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Chid Benz ameandika “NAVYOSEMA WATU WANA PESA ZANGU NAMAANISHA SIKURUPUKI. MTU HUFANYI NAE KAZI WALA HUNA NAE MKATABA WOWOTE NA ANATUMIWA YEYE PESA ZAKO NA ANAKUONESHA TUMEFIKIA HAPA.

HUFAHAMU HATA MOJA KUHUSU WEWE LAKINI UNALOFAHAMU NI MAINGIZO YANGU YA PESA. NIMEPIGA SIMU PIA KWA MDG WANGU MX LEO. NATAKA PESA ZANGU NA NAJUA WATU MNAZO. MIMI SIO CHIZI.

Mwisho ameandika BAADA YA KUMALIZA MATIBABU YANGU YA AFYA NAHITAJI PESA ZANGU. MUANZE TENA KUTISHIA KUNIPELEKA MAHAKAMANI. RASHIDI ABDALLAH MAKWILO.”

Mwanamuziki huyo amekuwa akidai kuwa kuna mtu alikuwa anatumia jina lake kwenda kuchukua pesa kwenye platform za muziki akijitambulisha kama meneja wa msanii huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *