Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amekanusha kuwa mjamzito baada ya kuonekana kuwa na muonekano wa umbo kubwa.
Kurasa kadhaa za udaku zilimfikia mwimbaji huyo kwa ujumbe wa pongezi, jambo ambalo lilimlazimu kujibu.
Katika moja ya jumbe hizo, Nandy alijibu kwa kejeli maswali ya kama ana mimba au la bila kukanusha au kukubali.
Kwa haraka, Nandy alijibu ujumbe wa shabiki huyo na kusema; “Kwamba huyo dada ana mimba anaifichaaaa yaaani hata sijui kwa nini anafanya hivyooo khaaaa…”
Shabiki mwingine alifika kwa mwimbaji huyo akimwambia kuwa mimba siyo ugonjwa.
Hii si mara ya kwanza kwa Nandy kulazimishwa kujibu tetesi za ujauzito.
Januari, mwaka huu, Nandy alikanusha tena madai kwamba alikuwa na ujauzito wa mchumba wake Billnass.
Nandy aliweka wazi kuwa, hakuwa na ujauzito na kuongeza kuwa atakapopata ujauzito habari hizo hazitafichwa kwa mashabiki wake kwani hazifichiki.
Wakati hayo yakiendelea, jana Jumapili lilikuwa ni tangazo la pili kanisani la Nandy na Billnass kutarajia kufunga ndoa Julai 16, mwaka huu.