Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso amefichua kuhusu bifu lake na mwenzake, Aslay huku akitupilia mbali madai kuwa chanzo cha tatizo lao ni wanawawake.
Mbosso amesema kuwa, hakuna sababu za msingi zilizosababisha ugomvi kati yao anasema kuwa, urafiki wao ulikatika ghafla tu baada ya Aslay kum-unfollow kwenye mitandao ya kijamii.
“Hakuna hata suala la maana ni upuuzi tu! Kitu gani cha maana hapo tulichogombania ni upuuzi tu kwamba huyu anafanya kazi zake huku na mwingine anafanya kazi zake huko, ghafla huyo wa huku kakunja na huyo wa huko kaona basi ikakuwa hivyo,” anasema Mbosso.
Mbosso anasema Aslay ndiye aliyetangulia kujitenga na Yamoto Band ili kuangazia kazi zake pekee yake baadaye, wanabendi wengine; Enock Bella, Beka Flavour na yeye, walitengana na kila mmoja akaanza kufanya kazi kivyake.
Mbosso amesema kuwa tofauti zake na mwenzake huyo wa zamani zilianza muda mfupi baada yake kujiunga na Lebo ya WCB iliyo chini ya Diamond Platnumz.