Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amefunguka na kusema kuwa hakuwa anatarajia mtoto ila mwili wake uliongezeka kutokana na kuridhika.

Kutokana Na Macho Ya Walimwengu Juu Ya Mwili Wake Nakuaminisha Kuwa Huenda Akawa Anatarajia Mtoto Kwa Kipindi Kile Msanii Shilole Ameweka Wazi Kuwa Kule Kulikuwa Ni Kunenepa Tu Na Sasa Ndio Rasmi Wapo Wanatafuta Mtoto.

 Pia Ameikataa Kauli Yake Aliyoitoa Miezi Saba Iliyopita kuwa Anatarajia Mtoto Na Kusema Kuwa Anakumbuka Ahadi Hiyo Kweli Lakini Sasa Ndio Wameanza Mchakato (Wakupata Mtoto)

“Mnanifuatilia Sana Mtu Asile Akashiba Wala Asiheme Niko Na Vitu Vingi Nina Shishi Food Nakula Vizuri, Napata Penzi Zuri, Sina Mkopo Ndio Maana Nanenepa So Kama Mlihisi Ni Mimba Ule Ulikuwa Ni Mwili Lakini Sasa Hivi Ndio Tupo Tunatafuta (Mtoto).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *