Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gigy amefunguka na kusema kuwa amemu Un-follow mwanamuziki mwenzake Malkia Karen Katika Ukurasa wake wa Instagram kisa kumpeleka Mtoto wake wa Miezi 8 Shule ya Bweni.
Gigy amesema kuwa Aliumia sana baada ya ya kuona Malkia Karen Ametangaza kuwa anampeleka Mtoto wake Shule ya Bweni ili aendelee kutafuta Maisha.
Amejitolea Mfano kuwa licha ya kuwa na Mambo mengi lakini hajawahi kufikiria Kumpeleka mtoto wake Marya kulelewa na mtu mwingine.
Gigy Money amesema kuwa anaumia sana kuona mama anakaa mbali na mtoto wake kutokana na upendo wake alionao kwa watoto.