Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mr Blue amesema hapati shida kuandika nyimbo kutokana na muziki kwake ni maisha, hivyo ni rahisi kupata ujumbe unaoihusu jamii anayoipelekea kazi zake.

Mr Blue amesema anaishi kwenye jamii inayoshabikia nyimbo zake, hivyo kuna wakati anakutana na matukio yanayomfanya aandike nyimbo zitakazowagusa wahusika moja kwa moja.

“Ninaposema muziki ni maisha ni kitu ambacho nakifanya kila siku, nitaimba, nasikiliza, nayaona matukio yanayofanyika kwenye jamii yapo ya kuburudisha na ambayo yanahitaji elimu”. amesema Mr Blue na kuongeza;

“Ndio maana sina presha nafanya kazi kwa kujiamini, kwani najua kila msanii ana jicho lake la kuyatafsiri matukio yaliopo duniani ama kwenye jamii zinazotuzunguka, kisha akaandika nyimbo”.

Pia amesema anafurahishwa na namna ambavyo chipukizi wanakuja kwa kasi, jambo ka msingi analowashauri wafanye kazi kwa bidii na wasiruhusu kiki zitawale muziki.

“Wapo chipukizi wengi wanaofanya vizuri, ninalotamani kuona kwao kazi zao ziongee sana kuliko kutawaliwa na kiki, mashabiki wanahitaji kupata burudani na elimu kupitia vipaji vyao na siyo maisha yao binafsi kuongelewa zaidi”. amesema Mr Blue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *