Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gigy Money amefichua siri ya mastaa wengi Bongo kuwa wana njaa inayowasababisha kuishia kuteswa na matumizi ya madawa ya kulevya (unga), bangi na pombe.

Gigy amesema kuwa kibaya zaidi hawana elimu ya matibabu ya kuondokana na msongo wa mawazo na kuishia kulalamika wasijue namna ya kujinasua huko.

“Mastaa wengi wa Bongo wanaishi kwenye njaa mpaka unawakuta wamepigwa picha wakiwa wamekondeana kwa sababu ya cocaine (unga), weed (bangi) na alcohol (pombe).

“Na kibaya zaidi Wabongo wengi hawajui kufanya therapy (tiba ya kuathirika na msongo wa mawazo) na ninamshukuru sana marehemu Ruge Mutahaba ndiye aliniambia ninahitaji mtu wa kuniweka vizuri kisaikolojia, therapist; mtu wa matibabu ya akili ni mambo ambayo wanapaswa kujifunza,” anasema Gigy

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la Pressure aliyomshirikisha Whozu ambaye inafanya vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *