Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefunguka na kusema kuwa kitu pekee anachokiangalia zaidi kwa sasa kwenye maisha yake ni furaha yake.

Kajala amesema kuwa anaangalia furaha yake ambayo ni muhimu kuliko makelele mengi ya waja yanayosikika kwenye mitandao ya kijamii.

Kumekuwa na kelele nyingi kutokana na kitendo cha kukubali kurudiana na ex-wake, Harmonize kwa kuwa kuna upande haukutaka hilo litokee.

Lakini Kajala amesema kuwa, ameamua kujipa furaha kwani hahitaji kujipa stresi wakati wote.

Kajala amesema kuwa, watu wanaweza wasimuelewe harakati zake, lakini ukweli ni kwamba kwenye maisha yake anaangalia zaidi ni nini ambacho anakifurahia na si watu wanachopenda yeye afanye, hicho ndicho kitu anachokiangalia zaidi kwa sasa.

Kajala amesema kuwa “Mimi naangalia zaidi furaha yangu kuliko kitu chochote kile kwenye maisha yangu hivyo ni vigumu sana mtu kunipangia furaha yangu iweje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *