Muigizaji wa Bongo Movie, Nicole amefunguka na kusema kuwa wanaume wanamuogopa kumtongoza ndio mana hadi leo ayupo kwenye uhusiano.

Nicole amesema kuwa, woga huo wa wanaume unatokana na yeye ni mzuri sana hivyo wanahofia gharama kubwa za kumtunza.

Nicole mwenyewe anawaondoa hofu kuwa yeye si mtu wa gharama kubwa kama wanavyomdhania kutokana na muonekano wake wa umbo.

Pia amesema kuwa wanaume wasimuogope kwani kwa sasa hata dereva bodaboda akija atamkubalia tu akiwa na upendo wa kweli kwenye mahusiano yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *