Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gigy Money amefunguka na kusema kuwa ametumia Tsh Milioni 32 kwenye usiku mmoja akisherehekea ‘Birthday Party’ yake akitimiza miaka 25.

Gigy Money amesema kuwa ameamua kutumia kiasi hicho cha pesa kwasababu ametimiza miaka 25 na ni furaha sana kwake kwa hiyo alikuwa haoni hasara.

Gigy Money amesema aligharamia kila kitu kwenye usiku huo kuanzia vyakula, vinywaji na ukumbi na pamoja na kugharamia usafiri wa baadhi ya wageni wake.

Baadhi ya mastaa walioalikwa kwenye sherehe hiyo kama vile Wema Sepetu, Mimi Mars, Lulu Diva, Amber Lulu na Baba Levo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *