Mwanamuziki na muigizaji wa Bongo Movie, Meninah amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake amepitia mambo mengi magumu mpaka hapa alipofika hivyo amejifunza vingi sana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Katika Safari Yangu Ya Maisha Nimepitia Vitu Vingi Sana Kwahiyo Vitu Vingine Vikitokea Naona Kawaida Unajua Mungu Akikupitisha Kwenye Dhoruba Hata Ukija Kupitia Kitu Gani Utaona Kawaida Tu, Siwezi Sema Nimepitia Matatizo Mengi Sana Kwasababu Nina Baraka Nyingi Sana Amabzo Watu Hawazijui’.

Ameendelea kuandika “Mimi Jambo Lolote Likinikuta Hata Kama Ni Baya Kiasi Gani Linaumiza Kiasi Gani Mimi Namshukuru Mungu Ndivyo Nilivyo Mwingine Anaweza Hata Kujiua Lakini Mimi Namshukuru Tu Mungu Kwasababu Nikiangalia Baraka Zangu Ni Nyingi Ambazo Wengine Hawana Na Maisha Yangu Pia Sio Mabaya”.

Pia ameendelea kwa kuandika “Kwahiyo Mshukuru Mungu Unaishi Kwako Hujapanga Una Maisha Yako Una Gari Unaendesha Unakula Familia Inasoma Shule Nzuri Hivyo Ndio Vitu Unatakiwa Kuwa Navyo Vingine Ni Mitihani Tu Mwenyezi Mungu Huitoa Kwa Mja Wake Ili Kumrudisha Kwenye Mstari”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *