Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baba Levo anajitanabaisha kama chawa (mpambe) wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz.

Staa huyo amekuwa akitoa kauli tata juu ya ukaribu wake na bosi wake huyo, Diamond Platnumz ambaye ni mmiliki wa Wasafi fm.

Baba Levo amewahi kusema kwamba angekuwa mwanamke kama Zuchu angemzalia watoto Diamond.

Hilo likapita, akasema Diamond ni baba yake na sasa ametoa kauli nyingine ambayo imeacha watu midomo wazi.

Baba levo anasema kwamba, kama ndugu zake watataka kuharibu ukaribu wake na Diamond, basi kuanzia siku hiyo atavunja undugu na hao wajomba, baba wadogo na wengineo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *