Mwanamuziki wa Singeli, Dulla Makabila ameachia wimbo wake mpya uitwao Naacha Mziki ambapo kwenye uandishi amezungumzia mahusiano yale na nyota wa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Makabila ameachia wimbo wake huo ikiwa ni siku chache tu tangu alipotuma ujumbe akimuomba msamaha Diamobnd Platnumz na uongozi wake ili kurejesha mahusiano mazuri yaliokuwepo kati yao.

Makabila kupitia uandishi wake kwenye wimbo huo amezungumzia anachoamini kuwa ni matokeo ya yeye kuwa mbali na Diamond pamoja na uongozi wake ikiwemo kuacha muziki na hatua alizochukua kuweka mambo sawa kati yao.

Mwanamuziki huyo kwasasa ameamaua kuomba msamaha kwa Diamond Platnumz baada ya wawili hao kutokuwa na maelewano mazuri kama ilivyokuwa hapo zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *