Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka na kusema kuwa alianza kazi hii kwa kuwaandikia wasanii wengi ngoma kali zilizotamba.
Marioo ambaye jina lake halisi ni Omari Mwanga anasema amezaliwa mwaka 1995 jijini Dar na akiwa bado mdogo, wazazi wake walimpeleka kuishi kwa bibi yake huko Rufiji mkoani Pwani.
Marioo kuingia kwake kwenye muziki kulitokana na kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na changamoto za kifamilia.
Anasema jina Mario (linatamkwa Marioo) limetokana na jina lake halisi ya Omari, akiitoa herufi ya kwanza O na kuipeleka mwisho wa jina.
Marioo amejizolea umaarufu baada ya kuwatungia ngoma wasanii wengi wakubwa kama Nampa Papa ya Gigy Money, Pambe wa Christian Bella, Nabembea wa Ditto, Bado ya Mwasiti, Sawa ya Msami na Wasikudanganye ya Nandy.
Wachache wanalitambua hilo kwamba hadi wale wakongwe kuna muda wanapungukiwa busara za kuandika mashairi hivyo kuomba msaada ili kuendelea kupeta kimuziki.