Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amefunguka na kusema kuwa hana masihara na mume wake hivyo hataki tatizo na mpenzi wake.
Shilole amesema kuwa hataki masihara kabisa na mume wake Rommy, ametangaza kumshushia mwanamke yeyote kichapo atakayeleta mazoea na mwanaume wake huyo.
Pia Shilole amesema kuwe na mipaka kwa mke na mume wa mtu kwa sababu hata yeye hana mazoea na wanaume za watu.
Mwanamuziki huyo kwasasa ameolewa na Rommy 3D baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake wa zamani Ashraf Uchebe.