Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bright amefunguka na kusema kuwa kabla ya kabla ya kuandika wimbo na kuachia, anazingatia mahitaji yaliyopo kwenye jamii husika.

Bright amesema kutokana na vipaji vya wasanii kuibuka kila kunapoitwa leo na ushindani kuwa mkubwa sokoni, jambo la msingi kwake ni kufanya muziki unaowagusa walaji wa kazi zake.

Bright amesema kuwa muziki unahitaji akili na kufanya utafiti mkubwa wa kujua unaowapelekea wanahitaji nini, hivyo vitu  ni muhimu zaidi kuliko kufanya ushindani usio na tija.

Ametolea mfano wa kibao chake cha Nitunzie alichomshirikisha Baraka the Prince, ndani yake kimebeba ujumbe wa mapenzi namna yanavyowaumiza wengi.

Baadhi ya nyimbo nyingine alizowahi kutamba nazo Bright ni Umebadilika aliomshirikisha Nandy, Mazonge kaimba na Jolie, Nakuja Dar kamshirikisha Stamina na Morogoro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *