Mtoto wa muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja aitwae Paula mara tu baada ya kusikia mama yake amerudiana na jamaa huyo, Paula aliamua kutomfuata mzazi wake huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kum-block kabisa, lakini sasa amelegeza kamba.

Kwasasa Paula amemsamehe mama yake na maisha yanaendelea na kuendelea na maisha yake kama zamani.

Hii ni baada ya Kajala kuendelea kushikilia msimamo wake wa kumrudia Harmonize na kukubali kupoteza hata watu wake wa karibu, lakini aendelee na maisha yake ya Konde Boy.

Watu wa karibu wamesema kuwa, ilikuwa ni lazima Paula akubali uamuzi wa mama yake na kutengua rasmi kile kiapo aliachoapa kwamba; “Labda nife!”

Katika sakata hilo, Kajala ameendelea kupokea lawama kama zote, lakini ameendelea kuwa imara huku akipewa magari ya kifahari aina ya Range Rover na kupewa cheo cha meneja kwenye Lebo ya Konde Gang inayomilikiwa na Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *