Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ambaye kama walivyo baadhi ya mastaa wengine wa kike, naye ameanzisha kuwa motivational speaker (mhamasishaji) kupitia nukuu zake.

Wema anasema kuwa, mwanaume bora si yule mwenye pesa nyingi, wala yule mwenye wanawake wengi, bali mwanaume bora na mzuri ni yule anayetambua thamani ya mwanamke.

Wema anaungana na wenzake kama Irene Uwoya, Shamsa Ford, Zamaradi Mketema, Lulu, Jacqueline Wolper na wengine wengi ambao wamekuwa wakitoa masomo ya aina hiyo.

Muigizaji huyo ameonekana kama muhamasishaji kwenye mitandao ya kijamii kutokana na anavyoziandika kila kukicha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *