Baada ya kuvunjika kwa kundi la muziki wa dansi nchini, FM Academia hatimaye kundi hilo limerudi tena na kufanya kazi kwa pamoja kama zamani.
Rais wa Bendi hiyo Nyoshi El Saadat amekiri kuwa tofauti yao ilikuwepo lakini sio kama watu wanavyodhani kwani wao ni kama ndugu na familia maana mara nyingi hushirikiana kwenye mambo mengi.
Ujio wa FM Academia unawakutanisha wakali wote waliyoitumikia Band kabla na Baada kukiwasha tena jukwaani Dar es Salaam mwezi ujao tarehe 02.
Bendi hiyo ilitamba miaka ya nyuma kutona na kufanya vizuri kwa vibao vyao mbali mbali vilivyoimbwa na wasanii wa bendi hiyo kama vile, Nyoshi El Saadat, Pacho Mwamba, Jose Mara, Pablo Masai pamoja na Mule Mule.