Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux na mrembo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe wameendelea kuwa gumzo mitandaoni kufuatia vitendo vyao vya mapenzi mubashara.

Kwa sasa Huddah yupo Tanzania siku chache tu baada ya kuahidi kuja kumtembelea Jux kwa lengo la kula naye bata.

Katika video aliyoposti Jux, Huddah anasema angependa sana kusalia kitandani na mwanamuziki huyo, Huddah anasikika akisema; “Mimi na mpenzi wangu tumetulia tu, sijui, ningependa kuwa kitandani na wewe.

“Ukiwa na Jux sasa unaenda wapi tena? Kwa nyumba nzuri hivi, natulia…”

Ikumbukwe hayo yanajiri baada ya Huddah kuuza sura kwenye video ya wimbo mpya wa Jux unaokwenda kwa jina la Simuachi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *