Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammedi Mchengerwa amesema “Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Tanzania imepanga kushirikiana na Asasi ya Viacom CBS Network Africa and Peer Lead BET International katika maandalizi ya Tuzo maarufu za Muziki Barani Afrika zinazojulikana kama MTV Africa Music Awards”

“Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Asasi ya Music in Africa Conference for Collaborations, Exchange, and Showcases (ACCES) yenye Makao Makuu yake nchini Afrika Kusini inaandaa Mkutano wa Wadau wa Muziki Afrika utakaofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Novemba, 2022”

“Majukumu mengine ni pamoja na kuratibu maandalizi ya mashindano ya urembo na Mitindo kwa Viziwi Duniani (Miss & Mr. Deaf International), kuratibu na kuandaa Tamasha la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival), matamasha saba (7) ya Kitaifa na Kimataifa, kusimamia programu ya Sanaa Mtaa kwa Mtaa; kuratibu uanzishwaji wa kikundi cha Sanaa cha Taifa kwa kushirikiana na BASATA, kuratibu mashindano ya Sanaa kwa vijana kupitia UMISSETA, UMITASHUMTA, Taifa Cup Music Challenge na Vyuo mbalimbali”

“Kuratibu ushiriki wa nchi katika Tamasha la JAMAFEST na kuunda Mfumo wa kupokea taarifa kutoka BASATA, BFT na COSOTA za usajili wa Wasanii, vibali vya kuendesha shughuli za Sanaa nchini, leseni za kutumia kazi za Sanaa pamoja na makusanyo na ugawaji wa mirabaha ili kuwa na kanzidata ya kisekta”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *