Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol licha ya muziki kuwa kwenye damu, haujamzuia kufanya shughuli zingine, ili kupanua kipato cha kujikimu maisha yake.
Ana madili mengi ikiwemo kufanya kazi na Umoja wa Mataifa (UN) kitengo cha hamasa kwenye maendelezo wa maendeleo endelevu (SDGs) na ni mkulima wa zabibu, mkoani Dodoma.
Amesema ndani ya muziki anakutana na fursa za kufanya kazi zinazongeza kipato, anachoamini kina nafasi ya kutunza heshima ya jina lake.
“Mimi ni kijana, nisipoichangamsha akili yangu kwa sasa uzeeni itakuaje, ndio maana nafanya kazi na mashirika mbalimbali kuhakikisha sitegemei muziki pekee kujipatia kipato,” amesema Ben Pol na ameongeza;
“Bado nalima zabibu mkoani Dodoma, hivyo kama kuna ukimya ukitokea nakuwa kwenye majukumu mengine.
Mbali na madili hayo, kesho Ijumaa ataachia nyimbo inayojulikana kwa jina la Piganisha, alioimba na wasanii wenzake Christina Shusho, Frida Amani na Joh Makini.
“Hiyo nyimbo inahusu uhifadhi wa mazingira, kesho Ijumaa tunaichia, kwa hiyo ukimya wangu haumanishi nimelala ama nimejisahau na kazi zangu hapana,” amesema.