Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu ameapa kupambania kombe kwa bosi wake, Diamond Platnumz.
Zuchu amekuwa akishindwa kuficha kabisa kuficha penzi lake kwa Diamond na jinsi ambavyo jamaa huyo ameweza kumnogesha.
Hata hivyo, Zuchu amekuwa akisemwa mno kwenye mitandao ya kijamii kuwa haendani na Diamond, hanogi wala kudamshi anapokuwa na jamaa huyo.
Katikati ya mjadala huyo, Zuchu ameibuka na kulitetea penzi lake hilo akisema; “Msione mtu anamng’ang’ani mtu, kuna vitu havielezeki.”
Hata hivyo, miezi sita baada ya penzi hilo, baadhi ya watu wanakiri kwamba Zuchu amembadilisha kwa kiasi kikubwa Diamond huku msingi mkubwa ukiwa ni kumsisitiza juu ya suala kumuogopa na kumcha Mungu kwa kumkumbusha sana suala la ibada.