Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa unapokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwaname utakiwi kuuliza mpo wangapi.

Linah ambaye siku hizi kama makali yake kwenye muziki yamepunua badala yake anafanya mambo kwenye tamthiliya.

Ili naye asisahaulike sana ameibuka na somo kwa watu wanaowapenda wenzake kimapenzi kwamba hawapaswi kuuliza wapo wangapi kwani hilo litajulikana kanisani au msikitini.

Linah ambaye ni mama wa mtoto mmoja anasema; “Ukimpenda mtu usiulize mpo wangapi, wewe unga foleni tu, mshindi atatangazwa kanisani au msikitini…”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *