Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amemualika Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya kutimiza miaka 30 toka aanze muziki.

Rais Samia amesema kuwa “Nimekubali kuwa hapa kwasababu Mimi ni Mama kwa Joseph sasa Mama kushuhudia mafanikio ya Mwanae ni fahari na leo nimeona fahari ya Kijana wangu”

“Sababu ya pili nimevutiwa na wazo la kujiandikia kitabu “Muziki na Maisha From The Street To The Parliament” sio wengi wanaopenda kuandika historia yao hasa ikiwa haina mwanzo mwema lakini nimevutiwa na uwazi alionao nikasema nakwenda kumsupport, na imempendeza nikizindue kitabu hiki na leo nitafanya hivyo”

“Kwa ninavyomfahamu Joseph nikiwa nae Bungeni, wengi watadhani ni Kijana machachari namkumbuka Bungeni siku amemuudhi Mh.Spika akasema mtoeni, Joseph na ufupi wake huo kashikwa mkono anatolewa kwahiyo Mtu mwenye picha ile atasema Joseph ni Mtukutu lakini kwakweli sio Mtukutu, ukipitia majina anayoitwa unaweza kusema Joseph ni Mtukutu lakini sio Mtukutu”

“Joseph amekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kwa vipindi viwili kupia CHADEMA na Mwenyekiti wake (Mbowe) yuko hapa na bila shaka Muziki ndio ulimuingiza Bungeni kwa kupata Wafuasi wengi hasa Vijana wamemwagia kura kaingia kwenye siasa, tuna mifano mingi ya Wanamuziki ambao wameingia kwenye siasa kama akina Prof.Jay, Mwana FA mmemuona hapa, Keisha yupo Bungeni na wengi wengine, mchango wa Joseph ni wa kipekee na amesaidia vipaji vya Vijana wengi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *